Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Uganda kupewa somo na Tanzania

Uganda kupewa somo na Tanzania

0 comment 117 views

Kamishna wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini ya Uganda Vincent Kedi amesema serikali nchini humo imetenga maeneo maalum ya madini ikiwa ni mojawapo ya mikakati yake ya kuiwezesha sekta hiyo kusaidia katika ujenzi wa taifa. Uganda imefikia hatua hiyo baada ya kuona mkakati huo ukifanikiwa nchi jirani za Tanzania na Rwanda. Mbali na kutenga maeneo hayo, serikali pia imejipanga kupeleka makundi mbalimbali ya uchimbaji madini katika nchi hizo ili wapate fursa ya kujifunza kuhusu mfumo huo kwa undani zaidi.

“Mfumo huu mpya utasaidia wachimbaji wadogo kujiunga na kuheshimiwa na wamiliki wa maeneo mbalimbali na kupunguza migogoro na upatikanaji haki katika maeneo hayo”. Ameeleza Kedi.

Kamishna huyo amesema mfumo huo umeonyesha mafanikio makubwa Tanzania na Rwanda, hali ambayo imepelekea serikali nchini humo kufikia uamuzi wa kupeleka viongozi wa makundi ya wachimbaji pamoja na kampuni ili wajifunze kwa undani.

Tanzania mbali na kutenga maeneo maalum yenye utajiri wa madini, pia imejenga pia uzio katika eneo pekee ambapo madini ya tanzanite hupatikana duniani kote, Mirerani mkoani Manyara. Kwa miaka mingi nchi haikuwa inanufaika na madini hayo lakini tangu uamuzi huo wa Rais John Magufuli, thamani ya rasilimali hiyo imeonekana. Awali, Kenya, India na Marekani zilisifika kwa biashara ya tanzanite japokuwa hazina madini hayo, hali inayoashiria yalichimbwa Tanzania na kuuzwa na kusafirishwa kiholela.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter