Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Hutaki kushindwa? Fanya hivi

Hutaki kushindwa? Fanya hivi

0 comment 107 views

Mara nyingi hatari ya kuanzisha biashara huwaogopesha watu hata kujaribu kuifanya biashara hiyo na badala yake kuendelea kubaki na wazo. Ieleweke kuwa vikwazo katika biashara humsaidia mfanyabiashara kukua na kufikia malengo yake kwani ikiwa biashara inaweza kustahimili vikwazo au hali ngumu ni rahisi kwa biashara hiyo kupiga hatua zaidi ili kufikia malengo.

Kufanya kazi kwa bidii na juhudi vinaweza kupotea kirahisi. Ili kuepuka hayo, unatakiwa kujenga mazoea haya:

Zingatia juhudi zako. Kutokana na maboresho ya teknolojia imekuwa rahisi kupata habari kuhusu namna ya kufikia malengo, jinsi ya kutoa huduma nzuri kwa wateja na kadhalika hivyo ni rahisi kukabliana na masuala hayo, lakini wewe kama mjasiriamali unatakiwa uzingatie zaidi malengo ya biashara ili kuepuka kushindwa. Weka kipaumbele zaidi katika kazi zinazohusu biashara yako,kuwa na mkakati madhubuti ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda kulingana na malengo yaliyopelekea biashara hiyo kuanzishwa vile vile ni muhimu kuwa na mfumo unaoeleweka. Hakikisha kuwa unajua wapi una ujuzi napo zaidi ili kuwapa watu wengine majukumu ili kazi ziweze kwenda.

Watu wa kujihusisha nao. Watu unaojihusisha nao wana ushawishi zaidi kuliko unavyoweza kufikiria. Marafiki, wanafamilia na hata washirika wana nguvu ya kubadilisha hisia, maamuzi na hata tabia. Kutumia muda hata kidogo kunaweza kubadilisha mtazamo na vitendo vyako vya baadae. Kuwa makini na watu unaojihusisha nao. Watu waliopo katika mtandao wako huleta uzoefu tofauti ambao husaidia katika hali mbalimbali hivyo tumia maarifa kujihusisha na watu ambao watasaidia kujifunza zaidi.

Unda utamaduni. Kama kiongozi unatakiwa kutengeneza hatua kwa ajili ya wafanyakazi kufanya kazi zao kwa uhuru ili mradi maslahi ya kampuni yanatimizwa. Weka taratibu na tamaduni ambazo zitasaidia kampuni iendelee na wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii zaidi.

Uza vitu vinavyohitajika. Duniani kuna bidhaa nyingi ambazo watu hawazihitaji, hivyo kupelekea wajasiriamali wengi kushindwa kwani hakuna soko. Wajasiriamali waliofanikiwa wamekuwa wakitengeneza bidhaa ambazo watu wako tayari kuzilipia. Kama mjasiriamali unatakiwa kujua kuwa kuna uhusiano mkubwa baina ya bidhaa na soko.

Uza kabla ya kutengeneza. Watu wengi hukosea pale wanapofikiria kuwa mawazo yao ni mazuri hivyo wateja watakuja tu kununua bidhaa au huduma zao. Kabla ya kuanzisha biashara ni muhimu kufanya majaribio ya kuuza. Wafuate watu ambao katika wazo lako ndio wateja wako na jaribu kuwauzia bidhaa yako ili kupata mrejesho utakaokufanya ufanye maamuzi sahihi.

Tengeneza mfumo. Sio rahisi kuwa na ufanisi bila kuwa na mifumo. Kukosa mifumo kutaleta changamoto katika kukuza biashara yako. Kwa mfano kama unataka kukuza mauzo yako unatakiwa kuwa na mfumo wa mauzo na masoko, kama unataka huduma bora kwa ajili ya wateja unatakiwa kuwa na mfumo maalumu wa huduma kwa wateja. Siku zote biashara bora hujengwa na mifumo maalum.

Aidha, kila kampuni/biashara huhitaji kiongozi lakini hiyo haimaanishi kiongozi awe mtu. Kampuni au biashara inatakiwa kuhakikisha inashindana katika dunia ya masoko kwa kutengeneza bidhaa yenye thamani kubwa kwa wateja. Ili kuepuka kushindwa, ni muhimu kuhakikisha thamani ni kubwa ili kuendelea kupata faida.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter