Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI IACHE PESA YAKO IKUTUMIKIE

IACHE PESA YAKO IKUTUMIKIE

0 comment 175 views

Ardhi ni moja kati ya rasilimali muhimu katika maisha ya binadamu.watu wengi wamekuwa wakiwekeza katika majengo kama njia mojawapo ya kujiingizia kipato. Wamiliki mbalimbali wa ardhi wamekuwa wakijenga majengo ya kuishi ama ya kibiashara na kupangisha katika miaka ya hivi karibuni. Uwekezaji huu unaonekana kuwa na faida kubwa japokuwa mmiliki nae hutumia gharama na muda mwingi kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa kabla ya kufanya biashara hiyo ya upangishaji.

Uwekezaji huu umeendelea kuwavutia watu wengi hususani vijana lakini kabla ya kuwekeza katika majengo ni muhimu kuwa na uelewa wa kina kuhusiana na biashara hii ili ikupatie faida. Watanzania wengi hawana desturi ya kujifunza kuhusiana na majengo kwa kina na hupendelea kuifanya kiholela bila ya kuweka akilini madhara ambayo yanaweza kutokana na uelewa mdogo wa kuwekeza katika majengo. Ikiwa unafikiria kufanya ujasiriamali huu, ni muhimu kuzingatia haya yafuatayo.

ADVERTISEMENT

Kwanza kabisa mmiliki anapaswa kufahamu kanuni na taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria. Tumeona sehemu nyingi hapa nchini zikikumbwa na adha ya bomoa bomoa hivi karibuni. Ni muhimu kwa yoyote anayefikiria kuwekeza katika majengo kuhakikisha kuwa sheria zilizopo hazimuwekei kikwazo chochote mahali anapotarajia kujenga kabla ya kuanza ujenzi. Watu wengi wamekuwa wakivunjiwa maeneo yao ya biashara kutokana na kwamba hawana uelewa wa kutosha wa sheria za nchi hivyo uwekezaji wao wote unapotea na kuwapatia hasara kubwa. Kuna umuhimu mkubwa wa kufuatilia taratibu zote za sheria ikiwa unafikiria kuwekeza katika majengo.

Tumia wataalamu ili kupata matokeo bora zaidi. Watanzania wengi hufanya kazi kwa mazoea wakiamini kuwa ni rahisi kumpa kazi mtu unayemfahamu bila kujali uzoefu na utaalamu wake. Hii inawaathiri wengi katika uwekezaji huu wa majengo. Ni vizuri wamiliki wajenge mazoea ya kutumia wataalamu waliobobea katika majengo ili mbali na kupata majengo yenye ubora pia wapate ushauri bora na kufahamu kwa undani zaidi kuhusiana na uwekezaji wao. Nyumba ni hitaji muhimu kwa binadamu na ni uwekezaji mzuri endapo utajenga kibiashara.

Ni muhimu kufanya utafiti kwenye eneo unalotarajia kufanya ujenzi kabla hujaamua kujenga. Hii itasaidia kutambua fursa na mambo hatarishi yaliyopo katika mazingira hayo na vilevile jinsi ya kuyatatua au kukabiliana nayo. Majanga ya bomoa bomoa, moto, mafuriko na vimbunga ndiyo yanayoathiri uwekezaji huu kwa kiasi kikubwa. Kabla ya ujenzi ni vizuri kujiridhisha juu ya eneo husika ili kulinda uwekezaji wako dhidi ya majanga mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter