Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Mhagama ashauri vijana kuanzisha vijiwe vya kiuchumi

Mhagama ashauri vijana kuanzisha vijiwe vya kiuchumi

0 comments 266 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuanzisha vijiwe vya kiuchumi. Waziri Mhagama ametoa ushauri huo katika ziara ya kukagua kituo cha maendeleo ya vijana, Sasanda mkoani Songwe.

Waziri huyo amesisitiza kuwa, serikali ya awamu ya tano imeendelea kutimiza azma ya kufikia uchumi wa viwanda na kuwataka vijana kutumia nafasi hiyo kujifunza na kuanzisha viwanda vidogo ambavyo vitabadilisha vijiwe walivyonavyo kuwa vya kiuchumi.

“Tunataka kuona vijana watakapojifunza kilimo bora, ufugaji wa ng’ombe au nyuki wataweza kuboresha thamani mazao na bidhaa kwa kuanzisha viwanda vidogo ndani ya mkoa wa Songwe, mkakati wetu katika kituo hiki ni kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana kuongeza thamani ya mazao na bidhaa watakazozalisha ambazo zitakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo yao””. Amesema Waziri huyo.

Aidha, Waziri huyo amewataka viongozi kushirikiana na ofisi yake, ili kuwasaidia vijana ambao tayari wameanzisha viwanda vidogo kwa kuwawezesha kuzalisha bidhaa bora na vilevile kuwatafutia soko ndani na nje ya nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!