Kiukweli sio rahisi kutengeneza fedha kwa haraka. Ikiwa unatumia njia ambazo hazivunji Sheria za nchi, basi ni muhimu kujituma, kujiamini na kufuata Sheria ili uweze kutengeneza kipato kwa sababu watu wamezoea kuwa njia ambazo sio za halali ndio huleta fedha kwa haraka, jambo ambalo si kweli.
Hizi ni njia tatu zinazoweza kukuletea fedha kwa haraka kupitia mtandao:
Kuuza vitu ambavyo hutumii
Hakuna maana ya kuwa na vitu vingi ambavyo huvihitaji. Unaweza kutengeneza fedha za haraka kuuza vitu ambavyo huvitumii. Kwa mfano unaweza kuuza nguo, viatu, mapambo, vifaa vya mazoezi, vifaa vya kielektroniki, makochi, magari n.k kwani kuna mitandao mingi ambayo inakuwezesha kufanya biashara hii kwa uharaka zaidi ili mradi bei iendane na vitu unavyouza na mteja aridhike na huduma inayotolewa
Kuuza ujuzi
Utandawazi umesaidia watu kuwasiliana kirahisi hivyo kama una ujuzi fulani ni rahisi kutengeneza fedha kupitia mitandao. Unaweza kutengeneza akaunti kwenye mitandao ya kijamii na watu wakajua kuhusu ujuzi wako na jinsi ya kupata huduma ya ujuzi wako. Pia kuna tovuti ambazo zimelenga kuwakutanisha watu na wataalamu wa masuala mbalimbali mfano Task Rabbit.
Watu kama wasusi, wapishi, wanamitindo na wachekeshaji wamenufaika na kuingiza kipato kizuri kutokana na kutangaza ujuzi wao kwenye mitandao.
Kuuza utaalamu
Kila mtu ana kitu ambacho anakifahamu kwa undani na kuna mtu mwingine anauhitaji wa jambo hilo kwa sababu hana uzoefu au amekosa elimu ya kutosha. Ndio maana kuna utakuta watu wameweka kwenye utangulizi kwenye akaunti zao za kijamii kuwa wao wanatoa ushauri (Consulting) wa jambo fulani kwa sababu wanakuwa wamebobea. Kutumia utaalamu wako ni njia nzuri ya kujiajiri.
Kama una utaalamu wa kutosha unaweza kujiajiri kupitia taaluma hiyo na kutengeneza fedha kwa sababu watu huwa wako tayari kulipa ili kujifunza mambo ambayo ni muhimu kwao.