Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bathow Mmuni ametoa wito kwa wajasiriamali kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo ikiwemo mikopo baada ya shirika hilo kuruhusu wajasiriamali kuwa wanachama kupitia vikundi vyao. Mmuni amesema hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali pamoja na wawakilishi kutoka benki mbalimbali zilizopo mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wajasiriamali wamesema kundi lao kupewa fursa ya kuwa wanachama wa NSSF mbali na kuwanufaisha kwa kuwapatia mafao na mikopo pia itasaidia kuwainua kiuchumi kwani wataweza kuendesha shughuli zao kwa ustadi zaidi. Naye Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema serikali inatambua mchango mkubwa walionao wajasiriamali katika kujenga taifa ndio maana inawatengezea mazingira mazuri na kuwaletea mafao ya NSSF.