Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Sido yatoa mafunzo kwa wasindikaji

Sido yatoa mafunzo kwa wasindikaji

0 comment 162 views

Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) mkoani Dodoma, Sempeho Manongi amesema shirika hilo linatoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kuhusu matumizi sahihi ya kemikali wakati wa usindikaji wa chakula na bidhaa nyingine ili kufikia ubora unaotakiwa na kumlinda mtumiaji wa bidhaa hizo.

“Malengo mengine ni kuongeza ushindani wa wajasiriamali katika kufikiria masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi, kuimarisha uwezo wa wasambazaji na watumiaji wa kemikali viwandani katika kuhakikisha matumizi endelevu yenye tija katika mnyororo wa uzalishaji na kuwajengea uwezo wazalishaji katika matumizi salama na bora na ya uhakika ya kemikali”. Amesema Manongi.

Meneja huyo ameongeza kuwa jiji la Dodoma lina wajasiriamali zaidi ya 2,000 ambao baada ya kukidhi vigezo vya ubora, wataweza kupanua zaidi wigo wa masoko huku wakiwa na uhakika wa usalama wa bidhaa hizo.

Naye, Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Dk. Engelbert Mbekenga amesema wamejipanga kutoa mafunzo ya usindikaji salama wa vyakula na matumizi sahihi ya kemikali wakati wa kutengeneza bidhaa mbalimbali, jinsi ya kufungasha bidhaa hizo pamoja na kuziwekea lebo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter