Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI ZEDO yawapa somo wajasiriamali

ZEDO yawapa somo wajasiriamali

0 comment 110 views

Afisa wa Bunge Francis John Songoro ametoa wito kwa wajasiriamali nchini kutumia elimu wanayopewa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kukabiliana na ushindani wa kimataifa. Songoro amesema hayo katika ufunguzi wa semina kwa wajasiriamali iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mfuko wa Tanzania (ZEDO) Ussi Suleiman ambapo alimuwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Afisa huyo ameeleza kuwa elimu ya ujasiriamali ikitumika ipasavyo, bidhaa zinazozalishwa nchini zitaweza kuuzwa katika soko la kimataifa na kuwashauri wajasiriamali kujikita zaidi kwenye kubuni mradi wa kuanza biashara.

“Tunatakiwa kuzalisha bidhaa bora zenye ushindani wa kimataifa, kupitia elimu hii itatusaidia kuzalisha vitu vizuri zaidi ya vile tulivyokuwa tunazalisha awali”. Amesema Songoro.

Akigusia suala la mikopo, Songolo amewataka wajasiramali kutumia vizuri mikopo yao ili waweze kuwa na uchumi wa kujitegemea badala ya kutumia mikopo hiyo kwenye matumizi yasiyotengeneza faida.

“Wapo baadhi wanakopa fedha badala ya kuzitumia fedha hiyo kwa malengo aliyokuwa ameyakusudia hafanyi hivyo badala yake anazipeleka kwenye vitu ambavyo hata siku moja haviwezi kukuza uchumi wake”. Amesisitiza Afisa huyo.

Naye Mwenyekiti wa ZEDO na Mkurugenzi Mfuko wa mikopo Tanzania, Ussi Saidi Suleiman amesema wametoa mafunzo hayo ili kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa ambazo zitaendana na soko la kimataifa.

“Katika mafunzo haya tumelenga kuwafundisha zaidi wajasiriamali kujua namna ya kubuni bidhaa ama biashara na pia tunatoa elimu ya ufugaji chura, mende pamoja na uchumi wa kijani”. Amesema Suleiman.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter