Home KILIMO Bashungwa: Nitawafuata wakulima mashambani

Bashungwa: Nitawafuata wakulima mashambani

0 comment 109 views

Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa amesema asilimia kubwa ya utendaji kazi wake hautafanyika ofisini na badala yake, atawafuata wakulima mashambani ili kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inakuwa na tija.

Bashungwa amesema hayo kwenye mkutano wa 15 wa sekta ya pamba mkoani Mwanza na kuwasisitiza watendaji wa wizara hiyo kuwajibika na kutatua matatizo yanayowakabili wakulima.

“Mimi niwahakikishie katika kipindi change sitakaa ofisini nitawafuata wakulima mashambani, tunao asilimia 65 ya watanzania wanategemea kilimo, hivyo hatuwezi kufanya mzaha na kilimo wakati huu wa serikali ya awamu ya tano”. Amesema Naibu Waziri huyo.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa wenyeviti pamoja na wakurugenzi watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga bajeti maalum itakayotumika kushughulikia na kutatua matatizo ya wakulima kwenye maeneo yao badala ya kutegemea kupata fedha hizo kutoka serikali kuu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, mikoa, wenyeviti wa Halmashauri, wakulima pamoja na wanunuzi wa zao la pamba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter