Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Cornel Masawe amesema kituo hicho kimetoa kiasi cha Sh. milioni 296.906 kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Makutupora mkoani Dodoma ambapo fedha hizo zimelenga kununua vifaa vya kisasa vya maabara ili kuiwezesha taasisi hiyo kufanya utafiti wa kilimo.
Kituo hicho kimepanga kuwawezesha wazalishaji wa mvinyo kwa kuwasaidia kutengeneza chupa zenye viwango na ubora unaokubalika viwandani.
“Tuna imani kuwa wakulima wakikitumia vizuri kituo hiki , kitasaidia kuzalisha zabibu na kuzalisha zabibu yenye sukari ya kiwango cha juu ambacho kimependekezwa ubora ili kuwezesha viwanda vya ndani kutengeneza mvinyo bora”. Amesema Dk. Masawe.
Kwa upande wake, Msimamizi wa makundi ya zabibu ya mizabibu ya kati, Richard Malle,ametoa wito kwa wakulima wa zao hilo kuwatumia wataalamu waliopo katika kituo hicho ili waweze kufanya kilimo bora cha zabibu.