Home KILIMOKILIMO BIASHARA Naibu Waziri Dkt. Biteko anadi soko la mazao jamii ya mikunde India

Naibu Waziri Dkt. Biteko anadi soko la mazao jamii ya mikunde India

0 comment 24 views

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ya Tanzania imejidhatiti kuboresha na kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuja na mipango kadhaa yenye lengo la kuongeza fursa kwa wakulima nchini.

Dkt. Biteko amesema hayo jijini New Delhi, India  wakati akishiriki mkutano kuhusu masuala ya mazao jamii ya mikunde.

“Tunaongeza uwekezaji katika utafiti na kuboresha upatikanaji wa teknolojia za kisasa za kilimo ambapo kila afisa wa ugani nchini amepewa vifaa vyote muhimu ikiwemo pikipiki na kompyuta ili kutoa huduma nzuri na kwa wakati kwa wakulima wetu,” Amesema Dkt. Biteko

Amesema Serikali pia imeboresha shughuli za usafirishaji wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kurahisisha michakato ya uuzaji mazao “Tanzania inaendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambayo itaimarisha usafirishaji wa bidhaa yenye urefu wa takribani kilomita 500 kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Dodoma ambayo imekamilika na na inatumika.

Vilevile, amesema kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) Serikali imewezesha vijana kwa kuwapa ardhi, fedha na upatikanaji wa masoko sambamba na kuongeza huduma za kifedha za kidijitali.

Aidha, Dkt. Biteko amesema “India ni soko muhimu kwa mazao jamii ya kunde kutoka Tanzania na tunaweza kupata mafanikio makubwa zaidi. Leo nawaalika wawekezaji kutoka India na nchi nyingine duniani kuja kuwekeza katika sekta ya kilimo ya Tanzania kuanzia uzalishaji wa kisasa wa soya hadi uwekezaji katika mifumo ya usimamizi wa mavuno.”

Akizungumzia maendeleo ya sekta mazao jamii ya mikunde, amesema kuwa mwaka 2023, Tanzania ilizalisha takriban tani 250,000 za mbaazi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 56 ikilinganishwa na mwaka 2018.

Inakadiriwa ifikapo mwaka 2030 Tanzania itakuwa na ukuaji mkubwa katika Pato la Taifa kupitia Kilimo, ambapo mauzo ya maharage mekundu, mbaazi na choroko yanatarajiwa kufikia dola bilioni 1.47, dola milioni 84 na dola milioni 115.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter