Home KILIMOKILIMO BIASHARA Rais Samia asisitiza kilimo biashara

Rais Samia asisitiza kilimo biashara

0 comment 83 views

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua vihenge, maghala ya kisasa na msimu wa ununuzi wa nafaka wa mwaka 2024/2025 katika Mkoa wa Katavi.

Wakati wa uzinduzi uliofanyika Julai 14, 2024 Rais Samia alisisitiza kuwa maghala haya ni kiashiria tosha kuwa kilimo cha sasa kinahitaji kubadilika na kuwa kilimo cha biashara badala ya mazao ya chakula pekee.

Aidha, alihimiza wakulima kuongeza uzalishaji ili kuwe na tija ya kibiashara.

Rais pia alielekeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuboresha zaidi teknolojia ya uhifadhi, na kujenga maghala zaidi ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi hadi kufikia tani milioni 3 mwaka 2030 ambapo Serikali imesema itahakikisha inaiwezesha NFRA kufikia malengo hayo.

Viongozi mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Anthony Mavunde Waziri wa Madini, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, Angela Kairuki ambae ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumaa Aweso Waziri wa Maji, Ummy Hamis Nderiananga Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Viongozi Wakuu Watendaji wa Mkoa wa Katavi.

Wengine ni pamoja na Dkt. Andrew Komba, Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Raymond Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bodi, Menejimenti na Watumishi wa NFRA; pamoja na wakulima na wananchi wa Mpanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter