Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tanzania yapata soko la mashudu ya alizeti China

Tanzania yapata soko la mashudu ya alizeti China

0 comment 65 views

Wakulima wa zao la alizeti pamoja na mazao mengine yakiwemo tumbaku, pilipili na parachichi wamehakikishiwa uwepo wa masoko ya mazao nchini China huku Serikali ikiendelea na juhudi za kufufua masoko katika nchi nyingine Duniani.

Akizungumza Agosti 14, 2024 mara baada ya kutia saini Hati ya Makubaliano ya Mauziano ya Mashudu ya Alizeti nchini China, iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde pamoja na Waziri wa Mamlaka ya Forodha ya Watu wa China Yu Jianhua katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar Es Salaam Silinde amesema makubaliano hayo yataongeza soko la zao la alizeti hapa nchini.

Ameeleza kuwa soko la Alizeti linapanda kwani baada ya kukamua mafuta wakulima na wafanyabiashara watapata mashudu ya kuyasafirisha kwenda China.

Ameongeza kuwa wamepata fursa ya mazungumzo ambapo nchi ya China imekubali makampuni takribani tisa kutoka Tanzania yanayoruhusiwa kusafirisha zao la parachichi, kusafirisha ambapo Tanzania itasafirisha bidhaa zake moja kwa moja kwenda China bila kumlazimu mkulima au mfanyabiashara kusafirisha kupitia nchi za jirani kama ilivyokua hapo awali.

“Kuna baadhi ya makubaliano ambayo bado yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji katika Serikali zote mbili. Yu Jianhua amenithibitishia kwamba watatuma timu yao kuja kuharakisha sehemu za makubaliano ikiwemo upelekaji wa pilipili nchini China zinakamilika pamoja na kuongeza usafirishaji wa zao la tumbaku nchini humo,” ameeleza Silinde.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter