Home KILIMOKILIMO BIASHARA WFP watakiwa kununua mahindi ya wakulima kwa Tsh. 700

WFP watakiwa kununua mahindi ya wakulima kwa Tsh. 700

0 comment 9 views

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewataka mawakala wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuhakikisha wananunua mahindi kwa wakulima kwa shilingi 700 kwa kilo.

Waziri Bashe amesema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Kituo cha Ununuzu wa Mahindi cha Kizuka, Mkoani Ruvuma Septemba 18, 2024.

Ameitaka WFP kununua mahindi moja kwa moja kwa wakulima kwa bei ya Tsh 700 au vinginevyo waende kununua mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Akiongea na wakulima waliokuwa anachekecha na kuchambua mahindi katika kituo hicho, Waziri Bashe amewaeleza wakulima hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ni sikivu na imeweka kipaumbele katika kutatua changamoto zozote walizonazo kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Wakulima hao walieleza changamoto zao ambao wengi wao wamevuna magunia zaidi ya 330 kwenye mashamba ya hekari 15.

Wakiongea mbele ya Waziri wameomba mawakala wanunue mahindi vijijini kwa angalau shilingi 600 hadi 650 badala ya shilingi 350 ambayo ni hasara kwao.

Pia wameomba miundombinu ya barabara na mawasiliano kutengenezwa, mashine za kisasa kuchambua mahindi, kuongezewa huduma za maafisa ugani na zana za kilimo na mbegu bora.

Akijibu changamoto kadhaa, Waziri Bashe ameeleza kuwa “nimeona uhitaji wa kuwa na mashine ya kisasa ya kuchambua na kusafisha mahindi. Nimeielekeza NFRA kununua mashine za kisasa za kuchambua mahindi ili kurahisisha huduma za Kituo hichi kwa wakulima.”

 

Wakulima hao pia wameelezwa kuwa wataongezewa maghala ya kuhifadhi chakula, mizani ya kidigitali, kujengewa Kituo cha Zana za Kilimo, kupatiwa mbegu za mahindi za ruzuku zikiwemo aina ya Hybrid na OPV, pamoja na mbolea za ruzuku.

Kuhusu miundombinu ya barabara na mawasiliano, Waziri Bashe ameeleza ataongea na viongozi wa sekta husika kwa ajili ya kusaidia ili kuongeza tija kwa wakulima.

Awali, Waziri Bashe alitembelea pia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambapo ameridhia ombi la Mkuu wa Mkoa kutumia shamba la Tumbaku la Ruvuma kuwa shamba la BBT kwa ajili ya matumizi ya wakulima waliopo karibu nalo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter