Home KILIMO Mashamba Morogoro yarudishwa serikalini

Mashamba Morogoro yarudishwa serikalini

0 comment 146 views
Na Mwandishi wetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba , Maendeleo na Makazi William Lukuvi amesema serikali imefuta umiliki wa mashamba makubwa 14 mkoani Morogoro katika wilaya za Mvomero na Kilosa baada ya wamiliki wao kushindwa kuyaendeleza ingawa wametakiwa kufanya hivyo kwa kipindi kirefu sasa na hata kuandikiwa barua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, Lukuvi amesema hatua hiyo imetokana na wamiliki hawa kushindwa kulipa kodi kwa takribani miaka mitatu sasa. Aliongeza kuwa miongoni mwa mashamba haya lipo ambalo awali lilimilikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye pamoja na mkewe Esther na shamba la Kampuni ya Noble Agriculture Enterprises.

Katika maelekezo ya Rais, baada ya shamba kufutwa umiliki, Mkuu wa Mkoa na Wilaya wanapaswa kuhakikisha kwamba mashamba hayo yanasimamiwa vizuri kwenye suala la ugawaji. Rais pia amewaonya viongozi wanaotaka kujimilikisha kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi watakapogundulika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter