Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wanaume 20 kupelekwa mahakamani kwa kuwapa mimba wanafunzi

Wanaume 20 kupelekwa mahakamani kwa kuwapa mimba wanafunzi

0 comment 73 views

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi mkoani humo Bw. Said Mtanda

Na Mwandishi wetu

Watuhumiwa 20 wanatarajia kufikishwa mahakamani mkoani Rukwa kwa tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi, na baada ya taratibu zote kukamilika wanaume hawa watafikishwa mahakamani mara moja.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi mkoani humo Bw. Said Mtanda amesema wilaya yake ipo katika vita kali dhidi ya mimba za mimba mashuleni na ameongeza kuwa zoezi hili ni endelevu ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Ili kuokoa wanafunzi wa kike ambao wengi wao hushindwa kuendelea na masomo sababu ya ujauzito, zoezi hilo limeanzishwa wilayani hapo na wanaume wenye tabia hizo wameonywa kuwa wakijulikana, watakamatwa na sheria itafuata mkondo wake.

Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kwamba hatovumilia tabia ya wazazi na walezi wa baadhi ya watoto kuharibu ushahidi wa kuwafikisha waliowapa mimba watoto wao mahakamani, amesema jambo hilo linashughulikiwa.

Hivi karibuni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwai alikamatwa baada ya kubainika alikuwa anafanya mpango ya kuharibu ushahidi na mtuhumiwa mmoja aliyempa mimba mwanafunzi mmoja shuleni kwake.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter