Home KILIMO Serikali yawekeza bilioni 751.1 kwenye kilimo 2022/23

Serikali yawekeza bilioni 751.1 kwenye kilimo 2022/23

0 comment 126 views

Serikali imewekeza jumla ya Tsh. 751.1 billioni katika sekta ya kilimo ikiwa ni sawa la ongezeko la asilimia 155.3% kwa mwaka 2022/2023 kutoka sh. 294.16 billioni ilizowekeza katika sekta hiyo mwaka uliopita.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2023-2027) (Medium Term Strategy) wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) pamoja na bidhaa za kifedha za Benki.

Amesema ongezeko hili kubwa linadhihirisha wazi nia ya Serikali kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo.

Amebainisha kuwa Serikali inafahamu umuhimu wa kilimo kwa uchumi wa nchi na kuutambua mchango wa TADB katika kutoa mikopo yenye riba nafuu kwenye kilimo na kuongeza kuwa Serikali itaendeleo kuwekeza kwenye kilimo.

Mwandumbya ameupongeza uongozi wa Benki hiyo pamoja na wafanyakazi kwa kukuza ufanisi wa Benki kwa kuongeza wigo wa huduma zake, huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono.

Mpango mkakati huo unalenga kuboresha kilimo nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter