Home KILIMO TADB yatoa matrekta kwa wakulima wa pamba

TADB yatoa matrekta kwa wakulima wa pamba

0 comment 112 views

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Japhet Justine amesema benki hiyo imetoa matrekta 24 yaliyo na thamani ya zaidi ya Sh. 1.5 bilioni kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Masoko (AMCOS) 24 vinavyojishughulisha na zao la pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa ili kuongeza tija na kuchochea uzalishaji wa zao hilo. Justine amesema wakati wa makabidhiano kuwa, TADB inalenga kuwawezesha wakulima hao ili wapate nafasi ya kuongeza uzalishaji kama inavyobainishwa katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).

 

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga amesema kupitia mkopo wa viuadudu uliotolewa msimu uliopita na benki hiyo na kusaidia wakulima zaidi ya laki sita wa pamba ulifanikiwa kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu uliopita. Mkurugenzi huyo pia ametoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana ili kusaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba hapa nchini.

 

Baadhi ya wakulima walionufaika na matrekta hayo wametoa shukrani za dhati kwa serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa matrekta hayo ambayo wamedai yataaidia kuongeza tija na uzalishaji wa zao la pamba hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter