• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Saturday, June 25, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Pato halisi la taifa kufikia 7.3% mwakani

“Serikali yetu imejipanga kuongeza kasi ya ukuaji wa pato halisi la taifa kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na matarajio ya asilimia 7.2 mwaka 2018 na kuongezeka kwa wastani wa asilimia 7.6 katika kipindi cha muda wa kati (2019/20 – 2021/22)” Amesema Dk. Mpango.

Patricia Richard by Patricia Richard
November 7, 2018
in FEDHA
0
Dk. Mpango amaliza utata ripoti IMF

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

Share on FacebookShare on Twitter

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema serikali imeweka mikakati ya kuongeza kasi ya ukuaji wa pato la taifa na kufikia asilimia 7.3 mwaka 2019 ikiwa ni moja ya shabaha na malengo ya uchumi jumla. Waziri Mpango amesema hayo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20

Katika maelezo yake, Dk. Mpango amesema kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, pato halisi la taifa lilikua kwa asilimia 8.4 ambapo kati ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kiwango kikubwa ni pamoja na ujenzi, habari na mawasiliano, usafirishaji na uhifadhi mizigo na kilimo.

“Serikali yetu imejipanga kuongeza kasi ya ukuaji wa pato halisi la taifa kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na matarajio ya asilimia 7.2 mwaka 2018 na kuongezeka kwa wastani wa asilimia 7.6 katika kipindi cha muda wa kati (2019/20 – 2021/22)” Amesema Dk. Mpango.

ADVERTISEMENT

Aidha, Waziri huyo ameweka wazi shabaha na malengo mengine ya uchumi, yakiwemo ya kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha unakuwa kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia 5 katika kipindi cha muda wa kati pamoja na mapato ya kodi kufikia asilimia 12.7 ya pato la taifa mwaka 2019/20 na kupita matarajio ya asilimia 12.5 mwaka 2018/19.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene ameishauri serikali kuanzisha utaratibu wa kutenga kiwango cha asilimia moja ya pato la taifa maalum kwa ajili ya shughuli za utafiti na maendeleo.

Tags: bungeDodomaPato la taifaPhilip Mpangouchumi
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Pichani ni matrekta yenye thamani ya zaidi ya Sh. 1.5 bilioni yaliyotolewa na TADB kama mkopo kwa AMCOS 24 zinazolima pamba kanda ya ziwa.

TADB yatoa matrekta kwa wakulima wa pamba

Discussion about this post

Habari Mpya

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 24, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 23, 2022

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 23, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 22, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 22, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 20, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 24, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

by Pesatu Reporter
June 23, 2022
0

Mapendekezo yamepitishwa kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo 23...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In