Home KILIMO Tizeba awaonywa wakulima wasiofuata sheria

Tizeba awaonywa wakulima wasiofuata sheria

0 comment 114 views

Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba amewaonya wakulima wanaolima tumbaku nje ya mfumo wa ushirika kama inavyoelekezwa na sheria ya zao hilo kuacha tabia hiyo mara moja kwani serikali itachukua hatua za kisheria dhidi yao. Waziri huyo amesema hao kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku ambazo zimefanyika kitaifa katika viwanja vya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mbali na kutoa onyo hilo, Dk. Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack kufanya kikao na wakuu pamoja na wakurugenzi wa wilaya zote mkoani humo kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu ya sheria ya zao la tumbaku. Ameongeza kuwa, tabia ya baadhi ya viongozi kuwakumbatia watu wanaofanya vitendo hivyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kupungua kwa wigo la soko la zao hilo.

Zao la tumbaku limekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa ambapo pato la mkulima limeongezeka kutoka Sh. 2,242,030 mwaka 2011/2012 na kufikia Sh. 5,982,745 mwaka 2016/2017.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter