Home KILIMO USDF yawapa tumaini wakulima kahawa

USDF yawapa tumaini wakulima kahawa

0 comment 99 views

Mfuko wa Maendeleo wa Kimarekani unaohudumia nchi za Afrika (USDF) umeamua kugharamia pembejeo na miche bora kwa wakulima wa kahawa zaidi ya 800 waliopo Kinyamvuo wlayani Moshi.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Kinyamvuo, Felix Mlay ameeleza kuwa shirika hilo limeshatoa Sh. 200 milioni kwa ajili ya kukarabati ofisi na maghala ya kuhifadhi kahawa na kununua miche bora. Kupitia fedha hizo, pia wataweza kununua pembejeo na kuwauzia wakulima hao kwa gharama nafuu ili waweze kulima kahawa zenye ubora wa hali ya juu.

“Wakulima watapata pembejeo na zitaweza kutolewa kwa mkopo na baadae mkulima atalipa kutokana na kahawa atakayouza, lakini pia miche mingi  ya kahawa imezeeka na tumepewa fedha kwa ajili ya kununua miche bora. Hii ni fursa kubwa kwetu katika kuboresha kilimo hiki ambacho wengi walishakikatia tamaa”. Amesema Mlay.

Ofisa Ugani wa kijiji cha Mwika Kinyamvuo, Devotha Assenga amesema bado wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima hao ili waweze kubadilisha miche ya  zamani na kunufaika zaidi na kilimo hicho.

“Tumeshaandika barua TaCRI ( Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania) kuomba miche ambayo haishambuliwi na magonjwa ya chulebuni na kutu ya majani”. Ameeleza Ofisa huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter