Home KILIMO Wakulima tumieni mitandao kujikwamua kiuchumi: TCRA

Wakulima tumieni mitandao kujikwamua kiuchumi: TCRA

0 comment 141 views

Wakulima nchini Tanzania wametakiwa kutumia fursa za mitandao katika kujikwamua kiuchumi ikiwamo huduma za masoko ya mazao wanayozalisha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka wakulima wanapoelekea kuadhimisha siku ya Wakulima (Nane Nane) kutumia mitandao ya kijamii kutangaza kilimo.

Akizungumza katika banda la TCRA, mkuu wa mamlaka hiyo kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Asajile John amesema matumizi bora ya mitandao yana faida kubwa ikiwa wakulima watatumia vizuri.
Amesema wanatamani kuona asilimia 80 ya watumiaji wa simu za mkononi wanafikiwa na huduma za mitandao.
Akizungumzia suala la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu amesema ni muhimu kwa kila Mtanzania kwa sababu itarahisisha huduma bora za mawasiliano.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter