Home KILIMO Wakulima wa miwa walamba mamilioni

Wakulima wa miwa walamba mamilioni

0 comment 119 views

Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amesema wakulima kumi na saba wa miwa kutoka wilaya ya Kilosa wamenufaika na urasimishaji mashamba kwa kutumia hatimiliki za kimila kukopa Sh. 550 milioni kutoka Benki ya Maendeleo ya Wakulima. Mgoyi amesema hayo wakati akifafanua kuhusu manufaa ya urasimishaji ardhi na mashamba, unaosimamiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita).

“Kwa kipindi cha miaka miwili wakulima 17 wa miwa huko Luhembe wametumia urasimishaji wa ekari zao 6,000 za miwa kupata fursa ya kukopa na hivyo wameongeza uzalishaji wa mavuno. Kama mtu alikuwa anavuna tani 15 hadi 20, sasa anavuna tani 35 hadi 40 na haya ni matokeo ya mitaji yao kukua kutokana na fursa ya ukopaji waliyoipata baada ya Mkurabita kuratibu urasimishaji wa mashamba yao na kwa msingi huo, pato lao limekua na hata pato la halmashauri yetu linaongezeka”. Ameeleza Mgoyi.

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa taasisi za fedha ikiwa ni pamoja na benki wilayani humo kuendelea kuzitambua hati za hatimiliki za kimila na kuzipokea kama dhamana ya mikopo kwa kuwa ni hati hizo ni halali kisheria na zinazotolewa na serikali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter