Home KILIMO Wakulima wa Mpunga wapata hasara ya mamilioni

Wakulima wa Mpunga wapata hasara ya mamilioni

0 comment 299 views
Na Mwandishi wetu

Mvua za masika zilizonyesha msimu uliyopita wa kilimo zimesababisha wakulima wa mpunga katika Bonde la Mto Ruvu mkoani Pwani kupata hasara baada ya hekari 800 za mpunga ambazo thamani yake ni Sh. 280 milioni kusombwa na maji.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Umwagiliaji wa Mpunga Ruvu (Chauru) Sadala Chacha amesema mvua hizo kubwa zilizonyesha zimepelekea wakulima kupata tani 6.5 badala ya tani 9 ambazo walikuwa wanategemea. Ameongeza kuwa heka zilizomwagwa mpunga mwaka huu zilikuwa 1,630 ambapo kati ya hizo, heka 800 zimesombwa na maji na heka 830 zilizobaki mpunga wake upo chini ya kiwango.

Mbali na hayo, Chacha ameongeza kuwa kwa msimu huu wa kilimo, wakulima hawana mbegu za kupanda kwani kitalu cha mbegu nacho kilisombwa na maji. Ameshauri wakulima kujipanga upya na kusubiria msimua wa kilimo wa mwaka 2018/2019.

Mwenyekiti huyo amesema ili kunusuru hasara hama hizi kwa siku zijazo, chama hicho kinapanga kuwakatia bima ya kilimo wanachama wake ili kuwasaidia wakati majanga kama haya yanapotokea. Chama hicho pia kinaangalia namna ya kutoa mikopo kama ushirika baada ya wakulima kudai kuwa kukopa benki kuna riba kubwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter