Home KILIMO Wakulima waruhusiwa kuuza mahindi nje

Wakulima waruhusiwa kuuza mahindi nje

0 comment 92 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema wakulima wapo huru kuuza mahindi nje ya nchi ikiwa wametoa taarifa serikalini. Majaliwa amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Lucy Mlowe aliyehoji serikali inatoa kauli gani kuhusu uwepo wa mahindi mengi yaliyokosa soko na hivyo kuwakosesha kipato wakulima nchini ikiwemo wa mkoa wa Rukwa. Majaliwa ameeleza kuwa Tanzania pia inaruhusu kuingiza mahindi ndani ya nchi ikiwa kuna vibali maalum kutoka mamlaka husika.

“Wakulima wanaruhusiwa kuuza mahindi nje ya nchi, jambo la muhimu hapa ni kuhakikisha kunakuwepo na taarifa sahihi ndani ya serikali ili tuweze kujiridhisha kama nchi ina chakula cha kutosha”. Amefafanua Waziri Mkuu Majaliwa.

Kuhusu uwepo wa viwanda vichache vya mbolea, Waziri Mkuu amekiri kuwa hali hiyo inapelekea bei ya mbolea kupanda zaidi huku akidai kuwa, serikali inatambua changamoto hiyo na tayari imefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Ujerumani ambao watajenga viwanda Kilwa na Mtwara, na viwanda hivyo vitaungana na kiwanda cha Minjingu ambapo uzalishaji wa mbolea utaongezeka na hivyo bei yake itapungua.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter