Home KILIMO Wakulima washauriwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa

Wakulima washauriwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa

0 comment 125 views

Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Issa Hamad ametoa wito kwa wakulima wa ukanda huo kuzingatia taarifa kuhusu hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hiyo kila siku ili kuepuka mabadiliko ambayo yanaweza kuleta athari katika kilimo chao.

Hamad amedai mamlaka hiyo imekuwa ikitoa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na hali ya upepo, kiwango cha mvua na unyevunyevu na kuwataka wadau kutoka sekta ya kilimo kuwa mstari wa mbele kuzitumia taarifa hizo.

“Serikali ya awamu ya tano inasisitiza kuzalisha kwa tija ili tuzalishe malighafi za kutosha kwa ajili ya kuendeleza viwanda, sasa taarifa zetu ni muhimu pia katika kuendeleza kilimo, endapo utabiri wetu utaonyesha kuwepo kwa mvua kidogo wakulima wanatakiwa kulima mazao ya muda mfupi, sasa wakulima wengi hawafanyi hivyo”. Amesema Hamad.

Mbali na wakulima, Meneja huyo amesisitiza umuhimu wa taarifa hizo kwa wale wanaosafirisha mizigo majini pamoja na wanaojishughulisha na uvuvi kwa madai kuwa, taarifa kutoka mamlaka hiyo itawasaidia kufahamu uwepo wa mawimbi makubwa na mabadiliko mengine.

Naye Meneja Masoko na Uhusiano wa mamlaka hiyo Rosemary Mchihiyo ameshauri wakulima kuacha kilimo cha mazoea na badala yake, watumie taarifa zinazotolewa na wataalamu ili waweze kuzalisha kwa tija na kuinua kipato.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter