Home KILIMO Walima ufuta wakusanya tani 14,000

Walima ufuta wakusanya tani 14,000

0 comment 157 views

Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale (Runali) mkoani Lindi Christopher Mwaya amesema chama hicho kimekusanya tani 14,463 za ufuta tangu msimu huo kuanza Juni mwaka huu ikiwa lengo lao ni kupata tani 18,000. Meneja huyo ameeleza kuwa waliweka lengo hilo wakiamini kuwa baadhi ya wakulima watauza ufuta moja kwa moja kwa wafanyabiashara badala ya kupitia vyama vya ushirika vya msingi.

“Huu ni msimu wa kwanza zao la ufuta kuuza katika mfumo rasmi wa kukusanya kwenye vyama vya ushirika na kuuzwa na kisha sisi chama kikuu kupokea taarifa za mauzo ya ufuta kutoka kwa maofisa wa vyama vya ushirika”. Amesema Mwaya.

Meneja huyo ameeleza kuwa bei ya ufuta imepanda kutoka Sh. 3,020 na kufikia Sh. 3,060 kulingana na soko huku akiamini kuwa wanaweza kufikia lengo lao la kukusanya tani 18,000 japokuwa msimu unakaribia kuisha. Meneja huyo amesema Runali inaendelea kuhamasisha kuwekeza nguvu zaidi katika kilimo hicho na kuepuka kuuza kwa wafanyabiashara kwa bei ambayo inawakandamiza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter