Home Elimu FAIDA ZA UBALOZI WAKO UNAPOKUA NCHI ZA KIGENI

FAIDA ZA UBALOZI WAKO UNAPOKUA NCHI ZA KIGENI

0 comment 221 views

Utume wa ki diplomasia(Diplomatic mission), ni  ujumbe wa watu unaotumwa kutoka nchi moja kwenda kuweka makazi ya kudumu katika nchi nyingine na kuwa muwakilishi pekee wa nchi aliyotoka.

Ubalozi(Embassy), ndio jina linalotumika kuitwa makazi ya wawakilishi hao, ambayo yanatakiwa yawe katika mji mkuu wa nchi hiyo iliyowapokea.

Makazi haya yanaongozwa na mtu anayeitwa balozi na eneo analofanyia kazi huyu kiongozi linaitwa kanseli na anapewa ulinzi na nchi iliyompokea.

Kuna mabalozi wengine wanalala hapo hapo katika kanseli na wengine wanalala nje ya kanseli lakini bado hata kama halali hapo,bado eneo analoenda kulala linapewa ulinzi na nchi iliyompokea.

Utume wowote wa umoja wa mataifa unaitwa utume wa kudumu(permanent mission) katika nchi husika na utume wa nchi za jumuiya ya Ulaya huitwa uwakilishi wa kudumu(permanent representation) kuongozwa na uwakilishi wa kudumu(permanent representative) na balozi.

Tume ya juu(High commission), ni jina linalopewa makazi ya wawakilishi wa nchi za jumuiya ya madola zikiongozwa na mtu anayeitwa kamishna.

Ubalozi mdogo(Consulate),hauna tofauti kubwa kiutendaji na ubalozi mkubwa japo wenyewe unawekwa nje ya mji mkuu wa nchi husika.

Na wenyewe  unajukumu la kushughulika na maslahi ya raia wao na biashara wanazofanya kwa ukaribu na unaongozwa na balozi mdogo.

Nchi moja yenye ubalozi katika nchi fulani, inaweza ikawa na balozi ndogo ndogo nyingi katika miji tofauti ikiwa imeona raia wa nchi yake wapo wengi katika miji hiyo.

Ubalozi wa nchi yeyote unapewa kinga ya kutobanwa na sheria za mitaa iliyopo.Na kutokana na agano la masuala ya diplomasia

lililoafikiwa Vienna na nchi zinazo pokea mabalozi,serikali ya nchi husika haziruhusiwi kuingia katika makazi ya ubalozi mpaka wapokee ruhusa kutoka kwa nchi yenye ubalozi wake.

Na hii ndio nafasi  pekee wanayoipata baadhi ya raia au wakimbizi wanapotakiwa kukamatwa na mamlaka ya nchi hizo,wakikimbilia ubalozini hawawezi kukatwa mpaka kwa ruhusa maalumu kutoka katika nchi yake.

Nchi za jumuiya ya madola zina kawaida ya kushirikiana shughuli za kibalozi,kwani kama nchi mojawapo yenye uanachama wa jumuiya madola ikiwa na ubalozi mahali utahusika kuhudumia pia raia wa nchi nyingine za jumuiya ya madola ambazo hazina ubalozi katika nchi hiyo.

Nchi zilizopokeana mabalozi zinapogombana hatua ya kwanza kuonyesha kwamba imechukizwa na jambo lolote liliofanywa na mmoja wao ni kumwita balozi wake nyumbani mpaka watakapofikia muafaka.

Ubalozi una fanya kazi kama zifuatazo:

  • Raia wa nchi yake amepatwa na matatizo ya pasipoti, iwe imeibiwa au kupotea wanahusika kumsaidia namna ya kupata nyingine.
  • Kumsaidia raia wa nchi yake anayetaka kwenda nchi nyingine kupata viza.
  • Kuisaidia nchi yake katika nyanja ya uchumi kwa kuwakutanisha wafanyabishara wa nchi yake na wa nchi uliyopo ili kufungua fursa za kiuchumi.
  • Unakuwa kama mpeleka ujumbe wa taarifa kubwa kutoka kwa kiongozi wa nchini kwake kwenda kwa kiongozi wa nchi uliyopo.

Na endapo umepatwa na tatizo unataka kukamatwa sehemu pekee ambayo ukiwa tu ndani ya uzio wake hakuna askari anayeruhusiwa kukukamata mpaka ruhusa itoke kwa balozi ni ubalozini.

Ubalozi ndio sehemu pekee ambayo inaweza  kukupa hifadhi hata mwezi mzima ili usikamatwe na pia unaweza ukakutorosha na kukurudisha nchini kwako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter