Home LifestyleTravel Serengeti yashinda tena

Serengeti yashinda tena

0 comment 128 views

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeendelea kung’ara baada ya kushinda Tuzo ya Hifadhi bora Afrika kwa mwaka 2023 (Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo.

Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ na kupokelewa na Mkuu wa Kanda ya Magharibi wa Tanapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Izumbe Msindai usiku wa Oktoba 15, 2023 katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE).

Serengeti imewashinda washindani waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ambao ni Hifadhi za Kidepo Valley National Park –Uganda, Central Kalahari Game Reserve- Botwswana, Etosha National Park -Namibia, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve – Kenya.

Ushindi huu unaifanya Serengeti kuwa Hifadhi bora zaidi Afrika kwa miaka mitano mfululizo yaani mwaka 2019, 2020, 2021, 2022 na 2023.

Tuzo za World Travel zilianzishwa mwaka 1993 ili kutambua, kutunza na kusherehekea ubora katika sekta zote muhimu ikiwemo sekta za usafiri, utalii na ukarimu.

World Travel Awards inatambulika duniani kote kama alama mahususi ya ubora wa tasnia mbalimbali.

Katika tuzo hizo, eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limetangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha kivutio bora cha utalii barani Africa (African leading tourist Attractions).

Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kushinda vivutio vingine vya utalii barani Afrika ambavyo ni table Mountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya afrika kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramis of Giza ya Misri.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter