Home Uncategorized CORONA kusimamisha shuguli EAC

CORONA kusimamisha shuguli EAC

0 comment 87 views

Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza kusitisha mikutano yote iliyopangwa kufanyika katika ofisi zake zilizopo Arusha kaskazini mwa Tanzania, kufutaia hofu ya maambukizi ya virusi vya corona iliyotanda kote ulimwenguni.
Tamko la Jumuiya hiyo linakuja katika wakati ambapo mkoa wa Arusha, yaliko makao makuu ya Jumuiya, kwa sasa unachukua tahadhari kubwa ya kujikinga na virusi hivyo baada ya kuripotiwa kwa visa kadhaa vya maambukizi katika nchi jirani ya Kenya, unayopakana nayo.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vicent Biruta, amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Liberat Mfumukeko, ya kusitisha mikutano yote inayojumuisha mikusanyiko mikubwa ya watu kutokana na hofu ya virusi vya COVID-19.
Taarifa hiyo inafafanua kwamba miongoni mwa mikutano iliyopangwa kufanyika hivi karibuni ni pamoja na mkutano wa 21 wa marais wa nchi wanachama uliokuwa ufanyika Jumatatu (16 Machi), huku mikutano mingine ikipangwa kufanyika kwa njia ya video.
Mpaka wa Namanga waimarisha ukaguzi
Katika hatua nyingine, tahadhari zaidi zimeendelea kuchukuliwa katika mpaka wa Namanga unaoziunganisha nchi za Kenya na Tanzania kufuatia visa vitatu vya corona kuripotiwa nchini Kenya.
Mkuu wa wilaya la Longido ulipo mpaka huo, Frank Mwaisumbe, alisema wilaya hiyo imeimarisha ukaguzi katika mpaka wa Namanga.
Wafanyabiashara wanaozunguka mpaka huo wanaeleza kuwa biashara zao zimeyumba hasa baada ya Kenya kutangaza visa vya corona.

Sara Keiya, mfanyabiashara wa shanga na urembo katika mpaka huo, aliiambia DW kwmaba wateja wengi kwa sasa hawawasogelei wafanyabiashara na “wafanyabiashara wenyewe wanaogopa kuwasogelea wateja kwa hofu ya kupata maambukizi ya corona.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter