Mabadiliko makubwa yametokea duniani kutokana na teknolojia. Na kila siku wataalamu wa masuala ya teknolojia wanaendelea kufanya maboresho zaidi katika mambo mbalimbali ili kuleta urahisi zaidi katika maisha ya binadamu.
Umeshawahi kujiuliza au kutaka kujua teknolojia zilizopo zilianzaje na waanzilishi walikuwa na malengo gani? Kuna mengi ambayo watu hawajui kuhusu mwanzo wa teknolojia zilizopo hasa zile maarufu.
Yafuatayo ni mambo matano ambayo wengi hawajui kuhusu teknolojia.
- Barua pepe iligunduliwa kabla ya intaneti
Inaelezwa kuwa barua pepe ya kwanza iligunduliwa mwaka 1965, na kutumika katika kompyuta ya MIT ambapo watumiaji wa kompyuta hizo walikuwa na uwezo wa kutuma na kupokea barua pepe kila wakati wanapoiwasha kompyuta hiyo. Mfumo wa intaneti ambao unaendelea kutumika hadi sasa ulikuja kugunduliwa mwaka 1971 na Ray Tomlinson.
- HP, Google ziligunduliwa katika gereji
Inaelezwa kuwa kampuni ya HP ilianzishwa katika gereji na waanzilishi wa kampuni hiyo David Packard na Bill Hewlett mwaka 1938 baada ya kupewa wazo na mwalimu wao kuanzisha teknolojia hiyo ya HP. Pia inaelezwa kuwa ofisi ya kwanza ya Google ilikuwa katika gereji. Google ilianzishwa na Larry Page na Sergey Brin. Vilevile kampuni ya Microsoft inaelezwa kuanzishwa katika gereji na Bill Gates mnamo mwaka 1975.
- Virusi vipya kila mwezi
Inaelezwa kuwa kila mwezi, virusi vipya 6000 katika vifaa vya kielektroniki hujizalisha.
- Ukubwa na uzito wa kompyuta ya kwanza
Inaelezwa kuwa kompyuta ya kwanza kutengenezwa ilikuwa na mita 2.5 kwenda juu na uzito wa kilo 30,000.
- Bei ya Hard disk ya kwanza
Mnamo mwaka 1980, kampuni ya IBM ilitengeneza hard disk ya GB 1 yenye ukubwa kama kinanda na kuiuza dola za kimarekani 40,000 ambazo ni zaidi ya milioni 90 za kitanzania.