Home VIWANDAMIUNDOMBINU Bilioni 12.6 zahitajika ujenzi barabara Dodoma

Bilioni 12.6 zahitajika ujenzi barabara Dodoma

0 comment 94 views

Kaimu Mratibu wa  Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Dodoma, Lusako Kilembe amesema kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Sh. Bilioni 12.6 zinahitajika kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya barabara jijini humo.

“Katika kutekeleza mpango huo, Wakala itatumia taarifa za utambuzi na hali halisi ya barabara mkoani, programu za matengenezo, mifumo ya utekelezaji pamoja na vipaumbele vilivyoainishwa katika kila halmsahuri” amesema Kilembe.

Hata hivyo ameeleza kuwa, kutokana na bajeti kuwa ndogo taasisi hiyo imeandaa mpango huo wa mwaka 2019/20 kwa kupitia vigezo kama mahitaji ya rasilimali fedha, mwenendo wa mahitaji ya uwekezaji na usalama wa watumiaji.

“Kwa kutambua ukomo wa bajeti, pia Wakala ilitumia vigezo maelekezo elekezi na vipaumbele vilitumika katika kuainisha barabara zitakazoingia katika mpango wa mwaka huu. Vipaumbele vikuu vilihusisha masuala ya kijamii,kiuchumi na kiufundi. Mapendekezo ya mpango wa mwaka 2019/20 yanahusisha mipango ya kazi za matengenezo inayogaharamiwa na mfuko wa barabara. Mpango huu pia unahusisha miradi ya maendeleo ambayo vilevile hudhaminiwa na mfuko wa barabara na wabia wa maendeleo”. Amesema Kaimu Mratibu huyo.

Bajeti hiyo ya Sh. bilioni 12.6 imetokana na majumuisho ya gharama katika maeneo ya; Bahi (Bilioni 1.035), Chamwino (Bilioni 1.44), Chemba (Milioni 863.90), jijini Dodoma (Bilioni 5.072), Kondoa Mjini (Milioni 711.27), Kondoa Vijijini (Milioni 966), Kongwa (Bilioni 1.53), na Mpwapwa (Bilioni 1.041).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter