Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Mnangagwa kutua nchini leo

Mnangagwa kutua nchini leo

0 comment 301 views

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajia kuwasili nchini siku ya leo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aingie madarakani Novemba mwaka jana. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, lengo la ziara hiyo ya siku mbili ni Rais Mnangagwa kujitambulisha kwa wananchi wa Tanzania.

 

Mbali na hayo, inatarajiwa kuwa ziara hiyo itaangazia zaidi masuala ya kiuchumi kwani nchi za Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu ya kiuchumi, kiplomasia, kihistoria na kijamii.

 

Zimbabwe inayokadiriwa kuwa na watu takribani Milioni 16.2 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2016 imekuwa ikitumia Bandari ya Dar es salaam kwa muda mrefu kusafirisha na kupokea bidhaa na mizigo yake mbalimbali.

 

Kiongozi huyo anatarajia kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli na baadae kutembelea Chuo cha sanaa Kaole kilichopo Bagamoyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter