Home VIWANDAMIUNDOMBINU TAA kuboresha huduma zake

TAA kuboresha huduma zake

0 comment 105 views

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Richard Mayongela, amesema wamejipanga kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya viwanja vya ndege nchini pamoja na katika kuhamasisha kasi ya utendaji ya wafanyakazi katika mamlaka hiyo. Mayongela ametoa ahadi hiyo mbele ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

“Kwa niaba ya wenzangu tunakuahidi kwamba kuanzia Januari mwaka inapoanza tutajitahidi kufanya kazi kwa weledi na kwa uadilifu mkubwa. Kwa upande wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere kuendelea kulalamikiwa kwa mambo madogo madogo ya kiutendaji haipendezi na ni aibu kwetu, mimi mwenyewe kama Mtendaji Mkuu nitachukua hatua na kuhakikisha kwamba tunakipa hiki kiwanja kipaumbele”.

Waziri Kamwelwe alianzia ziara yake katika kiwanja cha ndege cha Songwe na kugundua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege imejengwa chini ya kiwango na mkandarasi. Baada ya kutua JNIA, alibaini pia baadhi ya changamoto na kutoa maagizo kwa TAA kufanya mabadiliko ya kiutendaji kuanzia Januari mwakani.

“Nawaomba ndugu zangu kuanzia Januari mwakani mbadilike na kama mtu hatabadilika basi tutamtoa. malalamiko ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia myafanyie kazi”. Amesema Mhandisi Kamwelwe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter