Home KILIMO Mavunde: Zabibu utambulisho wa Dodoma

Mavunde: Zabibu utambulisho wa Dodoma

0 comment 145 views

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde ametoa wito kwa viongozi jijini Dodoma kuongeza nguvu katika uhamasishaji wa kilimo cha zabibu ili zao hilo liwe utambulisho kwa mkoa na taifa kwa ujumla. Mavunde amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoani humo (RCC) na kuongeza kuwa, zao hilo ndio pekee linaloweza kutambulisha mkoa na hata taifa kwani linavunwa mara mbili tu kwa mwaka.

“Tumekuwa na mazao ya kimkakati, korosho, pamba na zabibu kuna tofauti zao la mkakati na zao la utambulisho, utambulisho wa Dodoma ni zabibu, sababu ya upekee wake”. Ninaamini kuwa kilimo hiki kinaweza kubadilisha maisha ya wakulima na kuongeza hamasa ya kilimo cha zabibu”. Ameeleza Naibu huyo.

Aidha, Mavunde amesema amesikia kilio cha wachuuzi wa zabibu kuhusu kodi kubwa na kueleza kuwa kwa sasa, mchakato wa kupitia upya kodi hiyo ili zabibu zilete manufaa kwa mkulima unaendelea. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino, Musasa Kaweya ameshauri kuanzishwa kwa bodi ya zabibu ili kudhibiti soko na kuweka maizingira mazuri kwa wakulima kufaidika na kilimo chao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter