Home VIWANDANISHATI Eneo la mradi wa umeme Rufiji lakabidhiwa rasmi

Eneo la mradi wa umeme Rufiji lakabidhiwa rasmi

0 comment 112 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP), hatua ambayo inaashiria kuanza kwa ujenzi wa mradi wa umeme ambao unatarajia kuzalisha Megawati 2,115 zitakazoingizwa kwenye gridi ya taifa na kuiwezesha Tanzania kuwa na umeme wa uhakika.

Waziri Kalemani amekabidhi eneo la Hifadhi Matambwe lililopo mpakani mwa mikoa ya Pwani na Morogoro, kwa mkandarasi kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri. Amesema kuwa baada ya mradi huo kukamilika, bei ya umeme itashuka kwa kiasi kikubwa na hivyo kutasaidia nchini kutekeleza rasilimali muhimu za taifa.

Pamoja na hayo Dk. Kalemani amesema mradi huo utajenga bwawa kubwa, takribani mita za ujazo 34 bilioni pamoja na kituo cha kufua umeme ambacho kitakuwa na mashine tisa za kuzalisha umeme zenye uwezo wa megawati 2,115.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dk. Tito Mwinuka amesema mradi huo wa kihistoria, uliosainiwa kati ya shirika hilo na Kampuni ya Ubia Arab Contractors (Osman A. Osman Co na Elsewedy Electric), utakuwa na mkataba wa miezi 42.

Naye Msimamizi Mkuu wa kampuni hizo,, Makamu wa Rais wa kampuni hizo kutoka Serikali ya Misri, Wael Handy amedai mradi huo sio wa watanzania pekee, bali ni faida ya Afrika nzima.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter