Home VIWANDANISHATI Mikataba yote mafuta, gesi kupitiwa

Mikataba yote mafuta, gesi kupitiwa

0 comment 109 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema serikali imeanza zoezi la kupitia upya mikataba yote ya mafuta pamoja na gesi, ukiwemo mkataba wa Songas. Dk. Kalemani amesema hayo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kueleza kuwa, wamefikia hatua hiyo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Maalum ya Bunge.

“Kwa hiyo suala la kwamba mkataba wa Songas ufutwe, ufanyiwe maboresho au urekebishwe majibu yake yatatokana na mapendekezo ya kamati ambayo sasa marekebisho ya mapitio ya mikataba yanafanyika. Ni matumaini yetu matokeo ya mapitio ya mikataba yatakuja na uboreshaji wa mikataba hiyo ambayo nia ya watanzania ni kuhakikisha stahili ya watanzania inapatikana. Kwa hiyo niwaondoe wasiwasi wabunge kwamba, kwa vile mikataba inapitiwa upya kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni matumaini yetu mapitio haya yataboresha zaidi sio kwa upande wa Songas tu, bali kwa mikataba yote ya kuzalisha gesi pamoja na utafiti wa gesi na mafuta hapa nchini.

Mbali na hayo, Dk. Kalemani pia amezungumzia miradi mikubwa ya kuzalisha umeme na kusema kwa mara ya kwanza, Tanzania imetambulika kidunia kwa miradi mikubwa ya uzalishaji umeme inayoanzia Megawati 2,000.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter