Home VIWANDANISHATI REA III kunufaisha vijiji 35 Ngorongoro

REA III kunufaisha vijiji 35 Ngorongoro

0 comment 110 views

Naibu  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro William Olenasha amesema hadi kufikia mwaka 2019, vijiji 35 vitakuwa vimepata umeme wa REA III na baadae wataendelea na maeneo mengine. Waziri Olenasha ameyasema hayo katika kijiji cha Sakala alipofanya mkutano wa hadhara na wananchi na kusema kuwa, kila nyumba lazima itapata umeme na kuwasihi wananchi kuonyesha mwitikio mkubwa na kuichangamkia fursa hiyo yenye kuleta maendeleo.

Olenasha amesema kuwa tayari nguzo za umeme zimeendelea kupita katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha Ngorongoro inabadilika kuanzia miundombinu iliyopo mpaka mazingira ya watu ili kuhakikisha wanajenga Ngorongoro mpya.

Wote ni mashahidi hili hatuzungumzi tena, sio hadithi nguzo tayari zinasambaa katika vijiji na tunategemeaifikapo mwaka 2019 vijiji 35 vitakuwa na umeme.” Alisema Olenasha.

Kufuatia ziara hiyo, wananchi wamempongeza mbunge huyo kwa kuendelea kutekeleza ahadi zake na kuleta maendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter