Home VIWANDANISHATI Umeme wazidi kupenya vijijini

Umeme wazidi kupenya vijijini

0 comment 90 views

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amefika katika wilaya za Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua shughuli za usambazaji umeme vijijini ambapo amepata nafasi ya kuwasha umeme katika baadhi ya maeneo. Akiwa wilayani Handeni, Waziri huyo amewasha umeme katika kijiji cha Madebe, Nyasa na Kwamnele huku wilayani Lushoto, akizindua huduma hiyo katika vijiji vya Mabugai na Nkelei.

Viongozi kutoka wilaya ya Handeni wametumia nafasi hiyo kumtaarifu Waziri kuwa vijiji 10 ambavyo tayari vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini bado vinakosa nishati hiyo muhimu hivyo kusababisha malalamiko miongoni mwa wananchi ambao walitoka katika maeneo yao kupisha miundombinu hiyo. Kuhusu malalamiko hayo, Dk. Kalemani ameagiza wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanza utaratibu wa kupeleka umeme katika vijiji hivyo kwani miundombinu tayari ipo.

Waziri huyo pia ametoa onyo kwa meneja yeyote wa TANESCO atakayeonekana akitetea wakandarasi wanaochelewesha kazi kwa kisingizio cha kutokuwa na vifaa.

“Hawa wakandarasi tayari wameshalipwa fedha za kuwawezesha kuanza kazi ya usambazaji umeme vijijini, hivyo wanatakiwa kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika katika kazi hii”. Amedai Dk. Kalemani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter