Home VIWANDANISHATI Wakandarasi miradi ya umeme wapewa onyo

Wakandarasi miradi ya umeme wapewa onyo

0 comment 150 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameonya kuwa endapo mkandarasi aliyepewa dhamana ya kusambaza umeme vijijini akigundulika kufanya udanganyifu kwa wananchi na serikali kwa kutotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano, ataadhibiwa. Dk. Kalemani amesema hayo wilayani Gairo mkoani Morogoro alipotembelea kijiji cha Kibedya kwa ajili ya kukagua mradi wa usambazaji umeme na kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo.

“Nilipanga kuja hapa Disemba mwaka jana ndipo mkandarasi huyu akaamua kuleta umeme hapa, lakini sikuja na yeye akasimama kazi. Leo nimekuja kukagua na kukuta nyumba nyingi hazijaunganishiwa umeme na nguzo zimelala badala ya kusambazia watu nishati hii muhimu”. Amesema Waziri huyo.

Kufuatia hali hiyo, Dk. Kalemani amewataka mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wakandarasi wa umeme vijijini wanasambaza umeme katika maeneo yote waliyopangiwa, huku akisisitiza kuwa, mameneja wanaoshindwa kuhakikisha hilo wajiondoe kwa kushindwa kusimamia mradi inavyotakiwa.

“Ili kutekeleza mradi huu kwa kasi, naendelea kusisitiza agizo la serikali kila mkandarasi lazima awe na magenge matano ya kazi katika eneo lake ili kutorudisha nyuma juhudi za serikali za kuwasambazia umeme wananchi”. Amesema Waziri huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter