Home VIWANDANISHATI Watanzania washauriwa kuachana na matumizi ya mkaa

Watanzania washauriwa kuachana na matumizi ya mkaa

0 comment 70 views

Serikali imetoa wito kwa wananchi kutumia nishati mbadala na kuachana na matumizi ya mkaa ili kuepuka changamoto za uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea kote nchini. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Mbali na hayo, Makamba ameeleza kuwa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao yamebeba kaulimbiu inayosema “ Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala” yanalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu uharibifu wa mazingira pamoja na changamoto zake zikiwemo mafuriko na matumizi makubwa ya nishati ya mkaa.
Akifafanua zaidi kuhusu maadhimisho hayo, Makamba amesema  mwaka huu, siku ya mazingira itaambatana na kongamano la mazingira, mabadiiko ya tabianchi na uchumi ambalo litafanyika Juni 01 jijini Dar es salaam. Vilevile, ameshauri mikoa mingine kushiriki kikamilifu katka maadhimisho hayo ya mazingira.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter