Home VIWANDAUZALISHAJI Dkt. Mwinyi: wana CCM jivunieni mafanikio kwa maendeleo nchini

Dkt. Mwinyi: wana CCM jivunieni mafanikio kwa maendeleo nchini

0 comment 21 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa mafanikio ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) imeyapata ndani ya miaka 48 tangu kuasisiwa kwake ni kielelezo muhimu cha ubora wake na tofauti yake na vyama vingine vya siasa ndani na nje ya nchi.

Dkt. Mwinyi ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ameyasema hayo wakati akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Februari 05, 2025.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Wana-CCM wana kila sababu ya kujivunia mafanikio hayo kutokana na utekelezaji wa malengo ya chama katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Halikadhalika, Dkt. Mwinyi amewahimiza Wana-CCM kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na hatimaye kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao ili CCM ipate ushindi mkubwa na kuendelea kushika dola.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukiongoza chama hicho kwa umahiri na kuzisimamia Serikali zote mbili katika kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 kwa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa miaka 48 iliyopita baada ya kuunganishwa kwa vyama vya TANU na ASP mnamo tarehe 05 Februari 1977, tukio lililofanyika katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter