Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma ametoa wito kwa wanaolima viungo kuongeza juhudi na kuzalisha kwa wingi zao la vanilla kutokana na uhakika wa soko la bidhaa hiyo nje ya nchi. Waziri Juma ameeleza hayo wakati akijadili mikakati ya wizara kuzalisha mazao ya viungo ambayo mahitaji yake ya soko ni makubwa nje ya nchi.
Ameongeza kuwa tayari wizara ya kilimo kupitia mabwana shamba na wataalamu wake imeanzisha mashamba ya majaribio eneo la Kizimbani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutokana na utafiti uliofanywa kuonyesha kuwa mazao hayo yanastawi kwa wingi visiwani Zanzibar.
Waziri Juma ameorodhesha baadhi ya nchi zenye uhitaji mkubwa wa zao ikiwa ni China na Bara Hindi na Arabuni ambazo hutumia vanilla kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.
“Tumehakikishiwa soko la bidhaa mazao ya vanilla katika nchi ya China na Bara Hindi kwa hivyo wakulima kazi kwenu katika kuzalisha mazao hayo kwa mafanikio makubwa”. Amesema Waziri huyo.
Mbali na vanilla, ametaja mazao mengine ya viungo kama pilipili manga, bizari nyembamba, hiliki pamoja na pilipili hoho kuwa na soko kubwa