Home VIWANDAUZALISHAJI Vijana kutengewa maeneo ya uzalishaji.

Vijana kutengewa maeneo ya uzalishaji.

0 comment 108 views

Serikali kupitia Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu imewataka wakuu wa mikoa mbalimbali nchini kutenga maeneo maalum ya uzalishaji yatakayotumiwa na vijana hususan katika shughuli za uchakataji mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao hayo kuelekea Tanzania ya viwanda.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Antony Mavunde alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Arusha.

Mavunde amesema kuwa serikali itaendelea kuwawezesha vijana kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu sambamba na kuwapatia ujuzi utakaowatengenezea uwezo wa kujiajiri pamoja na kuajiri wengine. Aidha amewataka vijana kuwa wabunifu katika kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ambayo yamekuwa yakiharibika mashambani kutokana na ukosefu wa viwanda vidogo vya uchakataji.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema sera za serikali zinapaswa kuwa rafiki ili zitumike kuwawezesha vijana katika kujikwamua na kuondokana na umaskini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter