Home VIWANDAUZALISHAJI Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

0 comment 131 views

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali barani Afrika na inashika nafasi ya 14 dunia.

Ethiopia, ndio nchi inayoongoza kwa uzalishaji asali barani Afrika.

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki alibainisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya ushindi wa Tanzania kuandaa mkutano wa Dunia wa Ufugaji Nyuki (APIMONDIA).

Mkutano huo wa 50, unatarajiwa kufanyika mwaka 2027 jijini Arusha na kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki na utalii.

“Mkutano huo unakadiriwa kushirikisha wadau zaidi ya 6,000 toka mataifa mbalimbali dunia hivyo Tanzania kuwa mwenyeji wa kongresi hiyo kunatarajiwa kuleta manufaa makubwa ya kuchochea ukuaji wa sekta ya nyuki na uhifadhi, kuongeza mchango wa sekta katika pato la taifa, kuchochea utalii kwa ujumla nchini na kuvutia uwekezaji wa viwanda na teknolojia katika sekta ya ufugaji nyuki.

“Tumieni mkutano huu vizuri kwa kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki, kuongeza wigo wa mashirikiano na taasisi mbalimbali duniani katika kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo pamoja na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za ufugaji nyuki hususani teknolojia na mbinu mbalimbali za kuboresha na kuendeleza sekta hii,” ameeleza Waziri Kairuki.

Aidha, amesema mkakati wa Serikali kwa sasa ni ule ujulikanao kama “achia shoka kamata mzinga” ambao umelenga kudhibiti ukataji wa miti ovyo na badala yake kujikita katika kuongeza mizinga.
Hata hivyo, amesema kuwa kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa APIMONDIA Tanzania inakwenda kuwa nchi ya pili Barani Afrika kupewa jukumu hilo kubwa la kuandaa kongresi hiyo tangu kuanzishwa kwa APIMONDIA miaka takribani 130 iliyopita.

Kwa mara kwanza Kongresi hiyo kufanyika Barani Afrika ilifanyika nchini Afrika ya Kusini mwaka 2001.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter