Home WANAWAKE NA MAENDELEO Dkt. Biteko ataka fursa kwa mtoto wa kike ianzie katika ngazi ya familia

Dkt. Biteko ataka fursa kwa mtoto wa kike ianzie katika ngazi ya familia

0 comment 15 views

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameitaka jamii kuongeza nguvu ya kumpa fursa ya elimu mtoto wa kike kuanzia ngazi ya familia ikiwa ndiyo msingi wa maendeleo ya jamii.

Dkt. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam katika Kongamano lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communication “Citizen rising woman” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani machi 8, 2025.

“Tuanze nalo katika ngazi ya familia kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo katika jamii. Maendeleo ya jamii yeyote ile huanzia katika ngazi ya familia. Hivyo, sisi tumwendeleze mwanamke kwa kumpatia na kumfungulia fursa mbalimbali za elimu” amesema Dkt. Biteko.

Amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika maeneo kadhaa ikiwemo kuwawezesha wanawake kujikomboa dhidi ya umaskini, kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, kushiriki katika nafasi mbalimbali za maamuzi na hivyo kupiga hatua katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Wakati tunaposherehekea siku ya wanawake duniani, ni muhimu pia kusherehekea mafanikio tuliyopata katika kutatua changamoto za haki za wanawake hasa katika vipengele 12 vya Mwongozo wa mkutano wa Beijing” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, amesema wakati Duniani ina sherehekea Siku ya Wanaweke Kimataifa, kuna ulazima wa kutambua na kuzifanyia kazi changamoto zilizopo huku akizitaja baadhi yake kuwa ni ukatili wa kijinsia hasa maeneo ya vijijini, mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa wananchi na uelewa mdogo kuhusu masuala ya kijinsia hasa katika maeneo ya vijijini.

“Naomba niwakumbushe na maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa kwanza mwanamke kuwahi kutokea katika Taifa hili aliyoyasema mwaka jana katika hafla kama hii. Nanukuu “Ningependa kuona usawa wa kijinsia wa 50/50, lakini si kwa ajili ya takwimu tu, bali kuhakikisha wanawake tunasonga mbele, tukiwa na uwezo wa kuleta mabadiliko” mwisho wa nukuu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter