Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Mwinyi amesema serikali yake itafanya kila linalowezekana katika kuwasaidia wanawake kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uongozi wa kisiasa na uongozi katika utendaji.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanzawake Duniani Machi 8, 2022 yanayofanyika kitaifa Zanzibar, Rais Mwinyi amesema “tutaongeza idadi ya viongozi katika serikali”.
Aidha, Rais Mwinyi amesema serikali yake itaendelea kupinga udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
“Hapa Zanzibar udhalilishaji ni tatizo kubwa tunalopambana nalo na tukishirikiana tutashinda”.
Amesema serikali yake itakuwa mstari wa mbele kusaidia wanawake katika afya ikiwemo afya ya uzazi, mama na mtoto pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu inayosema “Zingatia usawa wa kijinsia ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi Zanzibar.