Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wahasibu wanawake 300 wanolewa

Wahasibu wanawake 300 wanolewa

0 comment 41 views

Takribani wahasibu wanawake 300 kutoka katika Halmashauri mbalimbali wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa fedha za umma.

Katika ufunguzi wa mafunzo hayo kwa wanawake wahasibu kutoka kwenye mafungu na Halmashauri iliyofanyika jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Jenifa Christian Omolo kwa niaba ya Katibu Mkuu Dkt. Natu El-maamry Mwamba amesema wahasibu hao wametakiwa kusimamia vizuri fedha za umma katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Omolo alisema Serikali inatarajia wahasibu hao watazingatia mafunzo yanayotolewa ili kuleta tija na kufikia lengo la Serikali la kuimarisha usimamizi wa fedha za umma.

Alisema katika mafunzo hayo wahasibu watajifunza kuhusu mawasiliano, masuala ya fedha na uwezeshaji wa kiuchumi, usimamizi wa wakati, namna ya utatuzi wa matatizo na maadili pamoja na afya ya akili.

“Mafunzo haya yatawaongezea uwezo mzuri katika mawasiliano kwa maandishi, mawasiliano ya kibinafsi na majadiliano kwa kukuza ujuzi wa kusikiliza na kuelewa mitazamo ya wengine.

Baadhi ya wahasibu wanawake wakiwa katika mafunzo.

Ujuzi wa mawasiliano kwa wanawake wahasibu itasaidia kujenga uhusiano mzuri, kukuza uwazi na mshikamano na kutatua migogoro mahali pa kazi na kwenye jamii,” alibainisha Omolo.

Omolo alisema elimu hiyo itawafanya wahasibu hao wawe na ujuzi stahiki wa usimamizi wa kifedha binafsi, kupangilia bajeti na matumizi, kuona fursa za uwekezaji na namna ya kuzitumia.

Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Ayoub Banzi kwa niaba ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Leonard Mkude, alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa wahasibu wanawake takribani 300 ambao ni sehemu ya wahasibu wanawake kutoka mafungu na Halmashauri zote za Tanzania Bara.

Alisema mafunzo hayo ni ya kwanza kutokewa katika mafunzo mengi ambayo wanatarajia kufanya ili kuendeleza na kuunga mkono juhudi za kumnyanyua na kumuwezesha mwanamke.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter