Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wanawake washauriwa kutumia mikopo kujiendeleza

Wanawake washauriwa kutumia mikopo kujiendeleza

0 comment 152 views

Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ametoa wito kwa wanawake jimboni kwake kutumia fedha za mikopo wanazopatiwa kujiendeleza katika masuala ya kiuchumi. Zungu ametoa ushauri huo wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali kuhusu namna ya kutumia mikopo kujiendeleza iliyoandaliwa na benki ya NMB. Mbunge huyo amedai kuwa benki ya NMB inafanya semina hiyo ili kutoa fursa kwa wanawake kujiendeleza na kuacha tabia ya utegemezi.

Takribani Sh. 4.5 bilioni zimepitishwa kwa ajili ya mikopo hiyo ambayo imewalenga wanawake, vijana na walemavu, kwa lengo la kuwawezesha kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kuleta maendeleo. Kwa upande wake, Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam Badri Idd amesema semina hiyo na utekelezaji wa mpango waliojiwekea hadi kufikia mwaka 2020.

“Tumeanza na kata 51 za Manispaa ya Ilala ili kuwezesha mpango wa serikali wa kuwawezesha wananchi kiuchumi uweze kukamilika kikamilifu”. Amesema Meneja huyo.

Katika semina hiyo, benki ya NMB imefanikiwa kufungua akaunti kwa vikundi 150 pamoja na akaunti binafsi 500 kwa wakazi wa mtaa huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter