Home FEDHA Faida za kuweka rekodi za kifedha

Faida za kuweka rekodi za kifedha

0 comment 118 views

Kuna umuhimu mkubwa kwa watu binafsi, kampuni, biashara na taasisi kuwa na utaratibu madhubuti wa kuweka kumbukumbu sahihi za kifedha. Haijalishi kiasi cha mapato ambacho mtu binafsi anakipata au kampuni inapata, kwa kuweka rekodi ya kumbukumbu za fedha ni rahisi kwa kuona maendeleo na kuchochea malengo kutimia.

Kwa kuwa na utaratibu wa kuweka rekodi ya matumizi ya kifedha kwa upande wa binafsi, za biashara nk unakuwa unajua ulipotoka na unapokwenda. Vilevile kwa kufanya hivyo unakuwa unajua mtiririko wako wa fedha, mambo gani ya kuacha na kuendelea ili kupata fedha zaidi, kama ni kwenye biashara au kampuni inakuwa rahisi kujua kama unapata faida au hasara na kutokana na kujua hilo, ni rahisi kufikia maamuzi ili kubadilisha muelekeo wako.

Kuwa na rekodi husaidia watu binafsi na biashara kujua sehemu ambazo zinatumia fedha nyingi zaidi. Kama sio matumizi muhimu, ni rahisi matumizi kufanya mabadiliko na  ikiwa matumizi hayo ni ya lazima inakuwa rahisi kuchukua hatua na kutafuta njia mbadala. Lengo kubwa la kuweka rekodi ni kuhakikisha unakwenda na bajeti, unafanya matumizi kutokana na uwezo wako na unapata mahitaji ya kila siku bila kuathiri mtiririko wa fedha.

Kwa upande wa biashara na ujasiriamali, kuwa na rekodi ya mapato husaidia katika upande wa malipo ya kodi na ushuru kwani ni muhimu kuandika matumizi yote hivyo ni rahisi kwa mfanyabiashara kufahamu mtiririko wake. Wafanyabiashara wanatakiwa kuhakikisha wanaweka rekodi sahihi ili kuepuka kupata hasara siku za baadae. Aidha, rekodi ya fedha ni muhimu kama unataka kukopa kwani mara nyingi wakopeshaji hutaka kujua mzunguko wa fedha ulivyo katika biashara hivyo kwa kuwa na rekodi nzuri, ni rahisi kupata mikopo na kujiendeleza.

Teknolojia imerahisisha mambo mengi ikiwemo kuweka rekodi ya mapato na matumizi binafsi na ya biashara. Unaweza kuweka rekodi ya mapato na matumizi yako kwa kutumia simu au kompyuta. Moja ya programu za kuweka rekodi ni SkyMkoba. Programu hii inaweza kutumiwa na watu binafsi, wafanya biashara, kampuni na taasisi za fedha.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter